Zaburi Sura 87
1
Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.
2
Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo.
3
Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu.
4
Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo.
5
Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.
6
Bwana atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo.
7
Waimbao na wachezao na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako.