Zaburi Sura 128
1
Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.
2
Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
3
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
4
Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
5
Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6
Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.