Zaburi Sura 6
1
Bwana, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2
Bwana, unifadhili, maana ninanyauka; Bwana, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3
Na nafsi yangu imefadhaika sana; Na Wewe, Bwana, hata lini?
4
Bwana urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5
Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7
Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8
Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa Bwana ameisikia sauti ya kilio changu.
9
Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu.
10
Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.