Zaburi Sura 13
1
Ee Bwana, hata lini utanisahau, hata milele? Hata lini utanificha uso wako?
2
Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?
3
Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4
Adui yangu asije akasema, Nimemshinda; Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5
Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6
Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.