Zaburi Sura 100
1
Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
2
Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
3
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4
Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5
Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.