Nawe, Ee Bwana MUNGU, umeniambia, Jinunulie shamba lile kwa fedha, ukawaite mashahidi; iwapo mji huu umetiwa katika mikono ya Wakaldayo; je! Itakuwaje?
Kwa maana kuna kujaribiwa; itakuwaje, basi, ikiwa upanga unaidharau hiyo fimbo? Haitakuwapo tena; asema Bwana MUNGU.
Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza?