kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hata kufikilia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikiliao hata Nea;
na Aiyaloni pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji minne.
Tena katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Taanaki pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji miwili.
Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la Bwana, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.
na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake;